Kituo cha Ufikivu

Kuleta ubunifu, ufikivu na kuhamasisha watu wote.

  • Taarifa ya Ufikivu
  • Kuelewa Ufikivu katika Spotify
  • Jinsi ya kuwasiliana nasi

Taarifa ya Ufikivu

Katika Spotify, tunasherehekea ubunifu wa binadamu na tunajitahidi kuhakikisha mfumo wetu unatumika na watu wote, ikiwa ni pamoja na mamilioni ya wasanii na mabilioni ya wasikilizaji. Kwa kujifunza kutoka kwa wataalamu na kuwaajiri watu wenye uzoefu wa masuala ya ufikivu, tunafanya kazi kuhakikisha bidhaa zetu zote zinazingatia ufikivu. Kwa pamoja, tunalenga kuwezesha kila mtu kuunda, kugundua na kuhamasishwa.

Jinsi ya kuwasiliana nasi

Kwa maswali yoyote, kama vile ufikiaji wa akaunti, malipo na hitilafu za kiufundi, tembelea tovuti yetu ya usaidizi au wasiliana na Huduma kwa Wateja.

Tumejitolea kukusanya maoni kuhusu ufikivu kutoka kwa watu ambao huenda wanatatizika kuhusiana na mojawapo ya yafuatayo:

  • Ufikivu wa maudhui, kwa mfano, "Siwezi kupata mistari ya nyimbo" au "Ninatatizika kufikia manukuu ya podikasti"
  • Ufikivu wa kidijitali, kwa mfano, "Siwezi kutumia teknolojia saidizi kwenye wavuti au programu"

Unaweza kuwasilisha maoni yako kupitia njia yoyote kati ya hizi:

Unaweza pia kuwasilisha maoni bila kujitambulisha kwa kutuandikia katika anwani iliyo hapa juu. Tutathibitisha tumepokea maoni yako, isipokuwa uyatume bila kujitambulisha.

Unapotoa maoni kupitia njia yoyote kati ya zilizoorodheshwa hapo juu (isipokuwa kupitia posta bila kujitambulisha), Spotify itakusanya, kutumia na kufichua maelezo yako ya binafsi kwa madhumuni ya kukagua na kujibu maoni yako, na vinginevyo itayadhibiti kwa mujibu wa Sera yetu ya Faragha.

Aliyeteuliwa kupokea maoni ya ufikivu ni: Msimamizi wa Mpango wa Timu ya Ufikivu.