Sera ya Vidakuzi ya Spotify

Itaanza kutumika kuanzia tarehe 29 Mei 2023

  1. Vidakuzi ni nini?
  2. Tunatumiaje vidakuzi?
  3. Chaguo za kudhibiti vidakuzi na matangazo yanayotokana na mambo yanayokuvutia
  4. Masasisho ya Sera hii
  5. Jinsi ya kuwasiliana nasi

Sera hii inafafanua jinsi Spotify inavyotumia vidakuzi. Kuanzia sasa, tutaiita 'Sera'. Madhumuni ya Sera hii ni kukupa wewe, mtumiaji wa huduma na/au tovuti za Spotify (kwa pamoja tutaziita hizi 'Huduma'), maelezo dhahiri kuhusu madhumuni ya Spotify kutumia vidakuzi na chaguo ulizonazo katika udhibiti wa mipangilio yako ya vidakuzi.

1. Vidakuzi ni nini?

Vidakuzi ni vipande vidogo vya matini vinavyopakuliwa kwenye kifaa chako, kwa mfano, unapotembelea tovuti. Vidakuzi ni muhimu kwa sababu vinaruhusu Spotify na washirika wetu kutambua kwa kipekee kifaa chako na kuwezesha matumizi yako endelevu, kwa mfano kwa kutusaidia kuelewa mapendeleo yako au vitendo vyako vya awali. Unaweza kupata maelezo ya jumla zaidi kuhusu vidakuzi katika: www.allaboutcookies.org.

2. Tunatumiaje vidakuzi?

Vidakuzi hufanya kazi nyingi tofauti, kama vile kukuruhusu kusogeza kati ya kurasa kwa ufanisi, kukumbuka mapendeleo yako na kuboresha kwa ujumla hali yako ya matumizi. Vinaweza pia kusaidia kuhakikisha kuwa matangazo unayoonyeshwa mtandaoni yanakufaa zaidi na yanaendana na mambo yanayokuvutia.

Spotify hutumia aina mbili kuu za vidakuzi: (1) vidakuzi ambavyo ni sharti vitumike; na (2) vidakuzi visivyo vya lazima:

  1. Vidakuzi ambavyo ni Sharti Vitumike

Vidakuzi hivi huwekwa na Spotify au mhusika mwingine kwa niaba yetu, na ni muhimu ili kukuwezesha wewe kutumia vipengele vya Huduma zetu, kama vile kuwasilisha maudhui kiufundi, kuweka mapendeleo yako ya mipangilio, kuingia katika akaunti, kufanya malipo au kujaza fomu. Bila vidakuzi hivi, Huduma zetu haziwezi kutolewa na hivyo huwezi kuzikataa.

  1. Vidakuzi visivyo vya Lazima

Vidakuzi visivyo vya lazima vinaweza kuwa 'vidakuzi vinavyohifadhiwa kwenye tovuti unayotembelea' au 'vidakuzi vya wahusika wengine tofauti na tovuti unayotembelea'. Vidakuzi vinavyohifadhiwa kwenye tovuti unazotembelea huwekwa moja kwa moja na Spotify au na mhusika mwingine kwa ombi letu. Vidakuzi vya wahusika wengine tofauti na tovuti unazotembelea huwekwa moja kwa moja na wahusika wengine au na Spotify kwa ombi la mhusika mwingine, kama vile watoa huduma wetu wa takwimu au utangazaji. Unaweza kuona orodha ya washirika hawa katika kiungo hiki. Spotify, au washirika wetu, hutumia vidakuzi visivyo vya lazima katika njia zifuatazo:

Aina ya Kidakuzi
Madhumuni
Vidakuzi ambavyo ni Sharti Vitumike
Vidakuzi hivi ni muhimu ili kukuwezesha utumie vipengele vya Huduma zetu, kama vile kuwasilisha maudhui kiufundi, kuweka mapendeleo yako ya mipangilio, kuingia katika akaunti, kufanya malipo au kujaza fomu. Bila vidakuzi hivi, Huduma zetu haziwezi kutolewa na hivyo huwezi kuzikataa.
Vidakuzi vya Utendaji
Vidakuzi hivi hukusanya maelezo kuhusu jinsi watumiaji wanavyotumia Huduma zetu. Kwa mfano, vidakuzi hivi huturuhusu kuhesabu idadi ya watu wanaotembelea tovuti yetu na kuelewa jinsi wanaotembelea tovuti yetu walivyoipata.
Takwimu za mtandaoni zinazotumia vidakuzi kukusanya data ili kuimarisha utendaji wa tovuti huwekwa katika aina hii. Kwa mfano, zinaweza kutumika kufanya majaribio ya usanifu na kuhakikisha mwonekano thabiti unadumishwa kwa ajili ya mtumiaji. Tunaweza pia kupata maelezo kutoka kwenye majarida yetu ya barua pepe au mawasiliano mengine tunayokutumia, ikiwa ni pamoja na iwapo ulifungua au kusambaza jarida au kubofya maudhui yake yoyote. Maelezo haya hutueleza kuhusu ufanisi wa majarida na kukusaidia kuhakikisha kuwa tunakupa maelezo yanayokuvutia.
Aina hii haijumuishi vidakuzi vinavyotumika kwa ajili ya mitandao ya utangazaji unaolenga mambo yanayowavutia/tabia za wanaolengwa.
Kiutendaji
Vidakuzi hivi huruhusu Huduma zetu kukumbuka chaguo unazofanya kama vile jina lako la mtumiaji, lugha au eneo uliko na kutoa maudhui na vipengele vilivyoimarishwa, vinavyokufaa zaidi. Kwa mfano, vidakuzi hivi vinaweza kutumika kukumbuka mabadiliko uliyofanya kwenye sehemu za kurasa za wavuti unazowekea mapendeleo.
Vidakuzi hivi hukumbuka chaguo ulizofanya ili kuboresha hali yako ya utumiaji. Usiporuhusu vidakuzi hivi, basi baadhi ya chaguo ulizofanya ulipotembelea Huduma zetu awali hazitahifadhiwa.
Vidakuzi vya ulengaji au utangazaji
Vidakuzi hivi hukusanya maelezo kuhusu tabia zako za kuvinjari ili kukuonyesha matangazo yanayokufaa zaidi na kuelewa mambo yanayokuvutia. Vitatumika pia kudhibiti mara ambazo unaonyeshwa tangazo na vile vile kusaidia kupima ufanisi wa matangazo yanayoshirikiwa na Spotify. Vidakuzi hivi huweka kumbukumbu kuwa umetembelea tovuti na maelezo haya yanaweza kushirikiwa na mashirika mengine kama vile watangazaji. Vile vile, Spotify inaweza kushiriki data chache na mifumo mingine ili kutangaza ofa, vipengele au matoleo mapya ya Spotify kwenye mifumo hiyo mingine. Usiporuhusu vidakuzi hivi bado utaonyeshwa matangazo lakini hayatawekewa mapendeleo mengi ili yakufae zaidi.

3. Chaguo za kudhibiti vidakuzi na matangazo yanayotokana na mambo yanayokuvutia

Mipangilio ya Kivinjari cha Wavuti

Unaweza kutumia mipangiio ya kivinjari chako cha wavuti kukubali, kukataa au kufuta vidakuzi. Ili ufanye hivi, fuata maelekezo yanayotolewa na kivinjari chako (kwa kawaida yanapatikana katika mipangilio ya 'Usaidizi', 'Zana' au 'Badilisha').

Tafadhali kumbuka kuwa ukiweka mipangilio ya kivinjari chako ikatae vidakuzi, huenda usiweze kutumia vipengele vyote vya tovuti ya Spotify. Ili upate maelezo zaidi, unaweza kutembelea www.allaboutcookies.org.

Vitambulishi vya Vifaa vya Mkononi

Kwenye kifaa chako cha mkononi, mfumo wako wa uendeshaji unaweza kukupa chaguo za ziada za kujiondoa kwenye utangazaji unaolingana na mambo yanayokuvutia au kubadilisha vinginevyo vitambulishi vya kifaa chako cha mkononi. Kwa mfano, unaweza kutumia mipangilio ya 'Ruhusu Programu Zitume Ombi ili Zifuatilie' (kwenye vifaa vya iOS) au mipangilio ya 'Jiondoe kwenye Matangazo Yanayolingana na Mambo Yanayokuvutia' (kwenye vifaa vya Android). Mipangilio hii hukuruhusu kudhibiti matumizi ya maelezo kuhusu unavyotumia programu zako kwa madhumuni ya kukuonyesha matangazo yanayolingana na mambo yanayokuvutia.

Utangazaji Unaolingana na Mambo Yanayomvutia Mlengwa

Huenda ukajiondoa ili usipokee matangazo yanayolingana na mambo yanayokuvutia kwa kuzima kidhibiti cha 'Matangazo yanayowekewa mapendeleo', kinachopatikana katika ukurasa wa Mipangilio ya Faragha ya Akaunti yako ya Spotify. Ukijiondoa ili usipokee matangazo yanayolingana na mambo yanayokuvutia kwa kutumia kidhibiti cha Matangazo yanayowekewa mapendeleo, Spotify haitashiriki maelezo yako na washirika wengine wa utangazaji au kutumia maelezo uliyotoa kwao kukuonyesha matangazo yanayolingana na mambo yanayokuvutia. Huenda bado ukapokea matangazo unapotumia Huduma kulingana na maelezo yako ya usajili kwenye Spotify na matumizi yako ya wakati halisi ya Spotify, lakini huenda yasikufae sana.

Baadhi ya matangazo yanayowekewa mapendeleo ambayo sisi, au mtoa huduma anayetoa huduma kwa niaba yetu, hukuonyesha yanaweza kujumuisha aikoni ya 'Ad Choices' au mbinu nyingine ya kujiondoa ili usipokee matangazo yanayolingana na mambo yanayokuvutia. Unaweza kubofya aikoni ya AdChoices au utembelee www.aboutads.info ili:

  • upate maelezo kuhusu ukusanyaji na matumizi ya maelezo kuhusu shughuli zako za mtandaoni kwa utangazaji unaolingana na mambo yanayokuvutia; au
  • ujiondoe ili data yako isitumike kwa utangazaji unaolingana na mambo yanayokuvutia na Digital Advertising Alliance (DAA) au kampuni zinazoshiriki.

4. Masasisho ya Sera hii

Huenda tukafanya mabadiliko katika Sera hii mara kwa mara.

Tunapofanya mabadiliko ya msingi kwenye Sera hii, tutakupa ilani dhahiri kama inavyotupasa kufanya katika hali hiyo. Kwa mfano, tunaweza kuonyesha ilani dhahiri ndani ya Huduma za Spotify au kukutumia barua pepe au arifa kwenye kifaa.

5. Jinsi ya kuwasiliana nasi

Asante kwa kusoma Sera hii. Ikiwa una maswali yoyote kuhusu Sera hii ya Vidakuzi, tafadhali wasiliana na Afisa wetu wa Usimamizi wa Data kwa kutumia maelezo ya fomu ya Usaidizi kwa Wateja kwenye Kituo cha Faragha au kwa kutuandikia kupitia anwani ifuatayo:

Spotify AB

Regeringsgatan 19, SE-111 53 Stockholm

Uswidi

SE556703748501

© Spotify AB.