Miongozo kwa Watumiaji wa Spotify
Hujambo! Karibu kwenye Miongozo kwa Watumiaji wa Spotify ("Miongozo kwa Watumiaji") ambayo ni muhimu unapotumia tovuti, programu na huduma za Spotify ambazo zinarejelea Miongozo hii ya Mtumiaji ("Huduma") ikijumuisha kufikia aina yoyote ya nyenzo au maudhui yanayopatikana kupitia Huduma hizo ("Maudhui" ) Miongozo hii kwa Mtumiaji imeundwa ili kuhakikisha Huduma zinaendelea kumfurahisha kwa kila mtu. Kando na Miongozo hii ya Watumiaji, maudhui lazima yafuate Kanuni za Mfumo wa Spotify ("Kanuni za Mfumo").
Tunaweza kusasisha Miongozo hii ya Watumiaji na Kanuni za Mfumo mara kwa mara - unaweza kupata toleo jipya zaidi kwenye tovuti yetu.
Kukiuka Miongozo ya Watumiaji au Kanuni za Mfumo kunaweza kusababisha kuondolewa kwa maudhui au nyenzo zozote ambazo umechangia kwenye Huduma na/au kusimamishwa au kufungwa kwa akaunti yako. Tunajaribu kuwezesha Huduma kupatikana kwa upana kwa kila mtu, lakini huwezi kutumia Huduma zetu ikiwa tulikuwa tumefunga akaunti yako awali kwenye Huduma zetu zozote. Pia tumepiga marufuku majaribio ya kukwepa hatua za awali za kisheria, ikiwa ni pamoja na kufungua akaunti mpya.
Vitendo vifuatavyo haviruhusiwi kwa sababu yoyote ile inayohusiana na Huduma na nyenzo au maudhui yanayopatikana kupitia Huduma hizi, au sehemu yake yoyote:
- kuiga programu, kuzalisha misimbo chanzo, kutafsiri misimbo ya mitambo, kurekebisha, au kuzalisha nakala za programu, isipokuwa katika hali ambapo kizuizi kama hicho kimepigwa marufuku wazi na sheria inayotumika. Iwapo sheria inayotumika inakuruhusu kuzalisha misimbo chanzo ya sehemu yoyote ya Huduma au Maudhui inapohitajika ili kupata taarifa muhimu ili kujenga programu huru inayoweza kuendeshwa na Huduma au pamoja na programu nyingine, taarifa unazopata kutokana na shughuli kama hizo (a) zinaweza tu kutumika kwa madhumuni yafuatayo, (b) haziwezi kufichuliwa au kuwasilishwa bila idhini iliyoandikwa mapema ya Spotify kwa wahusika wengine ambao si lazima kufichuliwa au kuwasilishwa kwao ili kufikia lengo hilo, na (c) kutumika kujenga programu au huduma yoyote ambayo inafanana kwa kiasi kikubwa katika asili yake na sehemu yoyote ya Huduma au Maudhui;
- kunakili, kuchapisha, kusambaza upya, "kunakili kwa programu," kurekodi, kuhamisha, kuwasilisha, kutunga, kuunganisha au kuonyeshwa kwa umma, kutangaza au kuwezesha kupatikana kwa umma, au matumizi mengine yoyote ambayo hayaruhusiwi wazi chini ya Makubaliano au sheria inayotumika, au ambayo inakiuka vinginevyo haki miliki;
- kuingiza au kunakili faili zozote za ndani ambazo huna haki ya kisheria ya kuingiza au kunakili kwa njia hii;
- kuhamisha nakala za Maudhui yaliyoakibishwa kutoka Kifaa kilichoidhinishwa hadi Kifaa kingine chochote kupitia njia yoyote;
- "kutambaa" au "kuchopoa", iwe inafanywa na mtu mwenyewe au kupitia njia za kiotomatiki, au vinginevyo kwa kutumia njia za kiotomatiki (ikijumuisha roboti, vichopozi na vitambaaji vya mtandaoni), ili kuona, kufikia au kukusanya maelezo, au kwa kutumia sehemu yoyote ya Huduma au Maudhui ili kufunza mfumo wa mashine kujifunza au muundo wa AI au vinginevyo, jinsi ya kuingiza Maudhui ya Spotify kwenye muundo wa AI au mfumo wa mashine kujifunza;
- kuuza, kukodisha, kutoa leseni ndogo, kupangisha au kuchuma mapato kwa njia nyinginezo isipokuwa kama inavyoruhusiwa wazi chini ya Makubaliano husika;
- kuuza akaunti ya mtumiaji au orodha ya kucheza, au kukubali au kupendekeza kukubali fidia yoyote, ya kifedha au vinginevyo, ili kuathiri jina la akaunti au orodha ya kucheza au maudhui yaliyojumuishwa kwenye akaunti au orodha ya kucheza; au
- kuongeza idadi ya uchezaji au ya wafuataji, kutangaza Maudhui kwa njia isiyo halali, au upotoshaji mwingine, ikijumuisha (i) kutumia mchakato wowote wa roboti, hati au wa kiotomatiki, (ii) kutoa au kukubali aina yoyote ya fidia (fedha au vinginevyo), au (iii) njia nyingine yoyote;
- kukwepa teknolojia yoyote inayotumiwa na Spotify, watoa leseni wake, au wahusika wengine, ikijumuisha vikwazo vyovyote vya ufikiaji wa maudhui vinavyotumika na Spotify au watoa leseni wake;
- kukwepa au kuzuia matangazo au kuunda au kusambaza zana iliyoundwa kuzuia matangazo;
- kuondoa au kubadilisha hakimiliki yoyote, alama ya biashara, au notisi zingine za uvumbuzi (ikijumuisha kwa madhumuni ya kuficha au kubadilisha viashiria vyovyote vya umiliki au chanzo);
- kufuta au kubadilisha sehemu yoyote ya Huduma au Maudhui isipokuwa inavyoruhusiwa wazi chini ya Makubaliano au, kwa Maudhui yanayotolewa na mtumiaji mwingine, kwa ridhaa ya moja kwa moja ya mtumiaji huyo; au
- kumpa nenosiri lako mtu mwingine yeyote au kutumia jina la mtumiaji na nenosiri la mtu mwingine yeyote.
Tafadhali iheshimu Spotify, wamiliki wa nyenzo na maudhui yaliyo kwenye Huduma hizi, na watumiaji wengine wa Huduma hizi. Usishiriki katika shughuli yoyote, kuchapisha Maudhui yoyote ya Mtumiaji, au kusajili au kutumia jina la mtumiaji, ambalo ni nyenzo au linajumuisha nyenzo ambazo:
- ni haramu, au zinanuiwa kukuza au kufanya kitendo haramu cha aina yoyote, ikijumuisha ukiukaji wa haki miliki, haki za faragha, haki za utangazaji, au haki za umiliki za Spotify au wahusika wengine, au zitakiuka makubaliano yoyote ambayo wewe ni mhusika, kama vile, kwa mfano tu wala si kuweka kizuizi, makubaliano maalum ya kurekodi au makubaliano ya kuchapisha;
- zinajumuisha nenosiri lako au nenosiri la mtumiaji mwingine yeyote kwa makusudi au zinajumuisha data ya kibinafsi ya wahusika wengine kwa makusudi au inakusudiwa kuchukua data hiyo ya kibinafsi;
- zinafichua taarifa za siri au za umiliki za mtu mwingine au maelezo ya kibinafsi kukuhusu ambayo hayakusudiwi kutangazwa kwa watu kote ulimwenguni;
- zinajumuisha maudhui hasidi kama vile programu hasidi, programu shambulizi za Trojan, au virusi, au vinginevyo huathiri ufikiaji wa mtumiaji yeyote kwa Huduma ya Spotify;
- zinaiga au zinawakilisha vibaya uhusiano wako na Spotify (ikiwa ni pamoja na, kwa mfano, kwa kutumia maudhui yenye hakimiliki ya Spotify, kutumia nembo ya Spotify bila ruhusa, au vinginevyo kutumia chapa za biashara za Spotify kwa njia ya kutatanisha), mtumiaji mwingine, mtu au shirika, au vinginevyo ni nyenzo ya ulaghai, uongo, udanganyifu au upotoshaji;
- zinahusisha uwasilishaji wa barua pepe nyingi zisizotarajiwa au aina zingine za barua taka, barua taka, barua mfululizo, au barua pepe za aina sawa;
- shughuli za kibiashara au za mauzo zisizoidhinishwa, kama vile utangazaji, ofa, mashindano, bahati nasibu, kamari, ubashiri wa spoti, au miradi ya piramidi;
- kuunganisha bila idhini, kurejelea, au kukuza bidhaa au huduma za kibiashara, isipokuwa kama ilivyoidhinishwa wazi na Spotify;
- zinaingilia au kutatiza kwa njia yoyote ile Huduma ya Spotify, kuathiri, kuvunja au kujaribu kuchunguza, kuchanganua, au kupima udhaifu katika Huduma za Spotify au mifumo ya kompyuta ya Spotify, mtandao, sheria za matumizi, au vipengele vyovyote vya usalama vya Spotify, hatua za uthibitishaji au hatua zozote za ulinzi zinazotumika kwa Huduma ya Spotify, Maudhui au sehemu yoyote yake;
- zinakinzana na Sheria na Masharti ya Spotify au sheria na masharti yoyote au sera zinazohusiana na matumizi yako ya Huduma zozote; au
- zimeondolewa kwenye huduma zozote zetu kwa kukiuka sheria na masharti au sera zetu, kama vile wimbo au kipindi kisichoruhusiwa. Hii ni pamoja na maudhui yanayoundwa au kubadilishwa ili kujumuisha upya au kutimiza lengo sawa na Maudhui yaliyoondolewa awali.