Katika Spotify, tunasherehekea ubunifu wa binadamu na tunajitahidi kuhakikisha mfumo wetu unatumika na watu wote, ikiwa ni pamoja na mamilioni ya wasanii na mabilioni ya wasikilizaji. Kwa kujifunza kutoka kwa wataalamu na kuwaajiri watu wenye uzoefu wa masuala ya ufikivu, tunafanya kazi kuhakikisha bidhaa zetu zote zinazingatia ufikivu. Kwa pamoja, tunalenga kuwezesha kila mtu kuunda, kugundua na kuhamasishwa.
Kwa maswali yoyote, kama vile ufikiaji wa akaunti, malipo na hitilafu za kiufundi, tembelea tovuti yetu ya usaidizi au wasiliana na Huduma kwa Wateja.
Tumejitolea kukusanya maoni kuhusu ufikivu kutoka kwa watu ambao huenda wanatatizika kuhusiana na mojawapo ya yafuatayo:
Ili kuwasilisha maoni bila kujitambulisha, usijaze sehemu ya anwani ya barua pepe na usitoe maelezo yoyote ambayo yanaweza kukutambulisha katika sehemu nyingine za fomu.
Tafadhali toa tu maelezo kuhusu ulemavu wako ambayo yanahusiana na maoni yako.
Aliyeteuliwa kupokea maoni ya ufikivu ni: Msimamizi wa Mpango wa Timu ya Ufikivu.