Masharti ya Ofa ya Mauzo ya Spotify Premium
Karibu kwenye Masharti ya Ofa ya Mauzo ya Spotify Premium. Kwenye ukurasa huu, unaweza kupata na kusoma sheria na masharti ambayo yanatumika kwa ofa ya mauzo ambayo umejiandikisha kwayo.
TAFADHALI SOMA MASHARTI HAYA KWA MAKINI NA KIKAMILIFU. YANA MASHARTI NA VIZUIZI KUHUSU UPATIKANAJI WA OFA ZA MAUZO ZA SPOTIFY PREMIUM NA TAARIFA KUHUSU MAMBO YANAYOTOKEA BAADA YA KUISHA KWA OFA YA MAUZO YA SPOTIFY PREMIUM.
1. Utangulizi.
Ofa za Mauzo za Spotify Premium (kila moja ni "Ofa ya Mauzo") zinawezeshwa kupatikana na Spotify chini ya Sheria na Masharti ya Spotify ("Sheria na Masharti ya Spotify").
Kila Ofa ya Mauzo inapatikana kwa njia ya Usajili wa Kulipiwa (kama inavyofafanuliwa katika Masharti ya Utumiaji wa Spotify), kama vile Spotify Premium Individual, Spotify Premium Student, Spotify Premium Family au Spotify Premium Duo kama itakavyokuwa na chini ya ofa kama ilivyotangazwa (kila moja "Huduma ya Spotify Premium").
Kulingana na Huduma ya Spotify Premium iliyotangazwa katika Ofa ya Mauzo, sheria na masharti haya ("Masharti ya Ofa ya Mauzo") huongeza na kuingiza kwa kurejelea sheria na masharti ya ziada yanayolingana na Huduma hiyo ya Spotify Premium, kama inavyoonyeshwa hapa chini:
Sheria na Masharti ya Huduma ya Spotify Premium yanayorejelewa katika Ofa ya Mauzo |
---|
Kwa Ofa yoyote ya Mauzo, iwapo kutakuwa na kutofautiana kati ya Masharti haya ya Ofa ya Mauzo na sheria na masharti yanayolingana yaliyorejelewa katika jedwali hapo juu, Masharti haya ya Ofa ya Mauzo yatashinda.
2. Ofa ya Mauzo.
Kila Ofa ya Mauzo hutoa ufikiaji kwa Huduma ya Spotify Premium iliyotangazwa:
- kwa bei iliyotangazwa (ikiwa ipo); na
- kwa kipindi cha utangulizi cha kwanza kama ilivyoelezwa zaidi katika kifungu cha 5 cha masharti haya, kuanzia wakati ambao unathibitisha kukubali Ofa ya Mauzo iliyotangazwa kwa kuwasilisha maelezo halali ya malipo ambayo yanakubaliwa na Spotify ("Kipindi cha Mauzo").
Kwa kuwasilisha maelezo yako ya malipo, wewe (i) unathibitisha kukubali Ofa ya Mauzo iliyotangazwa; (ii) unakubali na kukubaliana na Masharti haya ya Ofa ya Mauzo, pamoja na sheria na masharti husika yanayolingana na Huduma ya Spotify Premium iliyotangazwa (kama ilivyoelezwa hapo juu); na (iii) unatambua na kukubali Sheria na Masharti ya Spotify. Taarifa zote zilizokusanywa na Spotify chini ya Ofa yoyote ya Mauzo zitashughulikiwa na kutumiwa kwa mujibu wa Sera yetu ya Faragha. Isipokuwa zikitangazwa vingine, Ofa za Mauzo haziruhusu au kutoa ufikiaji kwa bidhaa au huduma zozote za mhusika wa Tatu.
3. Ustahiki.
Ili kustahiki kwenye Ofa ya Mauzo, watumiaji lazima watimize masharti yote yafuatayo (kila mmoja "Mtumiaji Anayestahiki"):
- Isipokuwa unajisajili kwa Ofa ya Mauzo ambayo inatangazwa kama inayopatikana kwa waliojisajili zamani kwa Huduma ya Spotify Premium, lazima uwe msajili mpya kwa aina yoyote na aina zote za Huduma ya Spotify Premium au Huduma isiyo na Ukomo (kama inavyofafanuliwa katika Masharti ya Utumiaji wa Spotify ) na usiwe umejiandikisha, au kukubali jaribio la, Spotify Premium au Huduma isiyo na Ukomo wakati wowote huko nyuma.
- Ikiwa unajisajili kwa Ofa ya Mauzo ambayo inatangazwa kama inayopatikana tu kwa waliojisajili zamani kwenye Huduma ya Spotify Premium, lazima uwe umejisajili kwa Huduma ifaayo ya Spotify Premium (kama ilivyotangazwa) ambayo usajili wake uliisha kabla ya tarehe ya kutangazwa.
- Kuhusiana na Ofa za Mauzo kwa Spotify Premium Student, Spotify Premium Family na Spotify Premium Duo: mahitaji ya ziada ya ustahiki yaliyowekwa katika sheria na masharti kwa mipango hiyo ya usajili.
- Isipokuwa ikitangazwa vinginevyo, toa kwa Spotify njia halali na ya sasa ya malipo ambayo inakubaliwa na Spotify (kadi za malipo ya mbeleni na kadi za zawadi za Spotify si njia halali za malipo).
- Isipokuwa ikitangazwa vinginevyo, toa njia ya malipo ya hapo juu moja kwa moja kwa Spotify na si kupitia mhusika wa tatu (k.v., si kupitia kebo au mtoaji wa mawasiliano ya simu au msambazaji mwingine).
- Mahitaji ya ziada ya ustahiki (ikiwa yapo) kama yanavyotangazwa mara kwa mara kuhusiana na Ofa ya Mauzo.
Watumiaji wanaostahiki wanaweza kukubali Ofa ya Mauzo mara moja - watumiaji wa awali hawawezi kukomboa ofa hiyo tena.
4. Upatikanaji.
Ofa ya Mauzo lazima ikubaliwe kabla ya tarehe ya kumalizika ya muda kutangazwa, ikiwa ipo. Isipokuwa pale inapokatazwa na sheria, Spotify ina haki ya kurekebisha, kusimamisha au kukatiza Ofa ya Mauzo wakati wowote na kwa sababu yoyote, katika hali hiyo hatutakubali uandikishaji unaofuta wa Ofa za Mauzo.
5. Muda na kughairi.
Kwa hali ya Ofa yoyote ya Mauzo, Kipindi cha Mauzo kinacholingana kitaendelea kwa kipindi ambacho kimetangazwa, kulingana na kifungu cha 4, hapo juu.
Isipokuwa ukighairi Ofa ya Mauzo kabla ya Kipindi cha Mauzo kumalizika, moja kwa moja utafanyika mtu anayejisajili mara kwa mara kwa aina ya Huduma ya Spotify Premium ambayo umechagua kujiandikisha chini ya Ofa ya Mauzo na njia ya kulipa uliyotoa itatozwa kiotomatiki bei ya kila mwezi ya wakati huo. Vipengele vyovyote vya wakati wa Huduma hiyo ya Spotify Premium vitapunguzwa kwa urefu wa Kipindi cha Mauzo
Iwapo umejisajili kwenye Usajili wa Kulipiwa unaotoa kipindi cha kwanza cha jaribio bila gharama kwako ("Jaribio la Bila Malipo"): iwapo utaghairi Jaribio la Bila Malipo wakati wa Kipindi cha Mauzo, utapoteza ufikiaji kwenye huduma ya Spotify Premium na akaunti yako ya Spotify itabadili hadi akaunti ya Spotify Free mara moja.
Iwapo umejisajili kwenye Usajili wa Kulipiwa unaotoa kipindi cha kwanza cha jaribio kwa gharama yoyote kwako ("Jaribio la Kulipiwa"): isipokuwa vinginevyo kama ilivyotajwa, kwa mfamo wakati wa mchakato wa kughairi, iwapo utaghairi Jaribio la Kulipiwa wakati wa Kipindi cha Mauzo, utapoteza ufikiaji kwenye Huduma ya Spotify Premium na akaunti yako ya Spotify ubabadili hadi akaunti ya Spotify Free mwishoni mwa Kipindi cha Mauzo.
Ili kughairi, lazima uingie kwenye akaunti yako ya Spotify na ufuate visituo kwenye ukurasa wa Akaunti au bofya hapa na ufuate maagizo.