Kituo cha Usalama na Faragha

Kanuni za Mfumo wa Spotify

Dhamira ya Spotify ni kuibua ubunifu wa mwanadamu – kwa kuwapa wasanii wabunifu milioni moja fursa ya kujipatia kipato kutokana na sanaa zao na mabilioni ya mashabiki fursa ya kufurahia na kuhamasishwa nazo. Tunaamini kuwa kutimiza dhamira hii kwenye mfumo wetu kunawezeshwa na hatua ya kukaribisha aina tofauti za kazi za sanaa, mawazo, mitazamo na sauti. Hii inaweza kumaanisha kuwa baadhi ya maudhui kwenye mfumo wetu huenda yasimpendeze kila mtu wala si maudhui ambayo Spotify inaidhinisha.

Hata hivyo, haimaanishi kuwa mfumo wetu unapokea kila kitu. Kando na masharti uliyokubali yanayosimamia utumiaji wako wa huduma zetu, kanuni hizi husaidia kuhakikisha kuwa kila mtu anapata matumizi salama na ya kufurahisha.

Je, kanuni hizi ni zipi?

Iwe wewe ni mwanamuziki, mtengeneza podikasti au mchangiaji mwingine, ni muhimu uelewe kuhusu maudhui yasiyoruhusiwa kwenye mfumo wetu. Mifano katika sehemu zilizo hapa chini ni kwa madhumuni ya kielelezo na siyo kamilifu.

Maudhui Hatari

Spotify ni makao ya jumuiya ambapo watu wanaweza kutayarisha, kujieleza, kusikiliza, kushiriki, kujifunza na kuhamasishwa. Usihimize ghasia, kuchochea chuki, kunyanyasa au kujihusisha katika tabia nyingine inayoweza kuwaweka watu katika hatari ya kupata madhara makubwa ya kimwili au kufa. Mambo ya kuepuka:

Maudhui yanayosifia au kuchochea madhara makubwa ya kimwili kwa mtu binafsi au kikundi ni pamoja na, ila si tu:

  • kuhimiza, kuhamasisha au kusifu vitendo vya kujiua au kujidhuru (ikiwa wewe au mtu mwingine unayemfahamu anatatizika au anawaza kuhusu kujidhuru, tafadhali angalia hapa ili upate njia za kupata usaidizi)
  • kuchochea au kutishia madhara makubwa ya kimwili au vitendo vya vurugu dhidi ya mtu mahususi au kikundi mahususi

Maudhui yanayochochea au kuunga mkono ugaidi au itikadi kali ni pamoja na, ila si tu:

  • kutukuza au kusifu vikundi vyenye itikadi kali au wanachama wake
  • kuratibu, kukuza, kutishia au kusifu kitendo cha vurugu kinachofanywa na au kwa niaba ya vikundi vyenye itikadi kali au wanachama wake
  • kutoa maelekezo au nyenzo za kufundisha jinsi ya kutekeleza kitendo cha itikadi kali
  • kushawishi mtu binafsi au kikundi kufadhili, kufanya kitendo cha itikadi kali au kujihusisha katika shughuli za kikundi chenye itikadi kali

Maudhui yanayolenga mtu binafsi au kikundi kinachotambulika ili kukinyanyasa au kukifanyia matendo mabaya yanayohusiana ni pamoja na, ila si tu:

  • kulenga mara kwa mara watu mahususi kwa matamanio ya ngono
  • kulenga mtoto mara kwa mara ili kumwaibisha au kumtishia
  • kushiriki au kushiriki tena maudhui ya kujamiiana bila ridhaa, pamoja na vitisho vya kusambaza au kufichua maudhui kama hayo
  • kushiriki, kutishia kushiriki au kuhimiza wengine kushiriki maudhui ya faragha ya mtu mwingine, ikiwa ni pamoja na maelezo ya kadi ya mikopo au ya benki, nambari za Kitambulisho cha Taifa, nk.

Maudhui ambayo yanachochea vurugu au chuki dhidi ya mtu au kikundi cha watu kwa misingi ya rangi, dini, utambulisho wa kijinsia au kujieleza, ngono, kabila, utaifa, mwelekeo wa ngono, hali ya kustaafu jeshini, umri, ulemavu au sifa nyingine zinazohusiana na ubaguzi wa kimfumo au kutengwa ni pamoja na, ila si tu:

  • kusifu, kuunga mkono au kuhimiza vurugu dhidi ya mtu au kikundi cha watu kulingana na sifa zilizoorodheshwa hapo juu
  • kauli za kukashifu mtu au kikundi kulingana na sifa zinazolindwa zilizoorodheshwa hapo juu
  • kuhimiza au kusifu vikundi vya chuki na picha na/au alama zinazohusiana navyo

Maudhui yanayotangaza maelezo ya matibabu ambayo ni ya uongo au danganyifu ya hatari yanayoweza kusababisha madhara nje ya mtandao au yana hatari ya moja kwa moja kwa afya ya umma ni pamoja na, ila si tu:

  • kudai kuwa UKIMWI, COVID-19, saratani au magonjwa mengine sugu yanayohatarisha maisha ni ya uongo au si ya kweli
  • kuhimiza ulaji wa bidhaa za blichi ili kutibu magonjwa mbalimbali
  • kuhimiza au kupendekeza kuwa chanjo zilizoidhinishwa na mamlaka za afya za eneo zimeundwa ili kusababisha kifo
  • kuwahimiza watu kuambukizwa COVID-19 kwa makusudi ili kujenga kinga dhidi ya ugonjwa huo (k.m. kukuza au kuandaa "sherehe za coronavirus")

Maudhui yanayotangaza kinyemela uuzaji wa bidhaa haramu au zinazodhibitiwa ni pamoja na, ila si tu:

  • kuuza silaha haramu au vipuri vya bunduki
  • kuuza dawa haramu
  • kuuza spishi zilizo hatarini kutoweka au bidhaa zinazotokana na spishi zilizo hatarini kutoweka

Maudhui yanayotangaza, kuomba au kuwezesha dhuluma au unyanyasaji wa watoto kingono ni pamoja na, ila si tu:

  • picha zinazoonekana za mtoto anayejihusisha katika kitendo cha ngono au maonyesho ya wazi sana ya mtoto akiwa uchi
  • kuhimiza vitendo vya unyanyasaji wa kingono dhidi ya mtoto ili kumpa pesa
  • kuhimiza au kutangaza mvuto wa kingono wa watu wazima kwa watoto
  • kuhimiza, kurahisisha kuwa kawaida au kusifu vitendo vinavyomkuza mtoto katika matendo ya ngono

Maudhui ya Udanganyifu

Kuwezesha hali nzuri za matumizi kwenye Spotify kunahitaji imani kuwa watu wanajitambulisha bila hila, kuwa hawatalaghaiwa na kuwa hamna anayejaribu kuchezea mfumo wetu kwa njia za udanganyifu. Usitumie mbinu danganyifu ili kuwahadaa wengine. Mambo ya kuepuka:

Maudhui yanayoiga wengine ili kuwahadaa ni pamoja na, ila si tu:

  • kunakili jina, picha na/au maelezo yale yale ya mtayarishi mwingine aliyepo
  • kujifanya kuwa mtu mwingine, biashara au shirika kwa njia ya kupotosha

Maudhui yanayotangaza nyenzo za kutunga na zisizo halisi kama zilizo halisi katika njia zinazoleta hatari ya kupata madhara ni pamoja na, ila si tu:

  • rekodi ya sauti au video inayotoka kwenye chanzo halisi na halali ambayo imebadilishwa katika njia ambayo inabadilisha maana au muktadha wa maudhui halisi na inayodaiwa kuwa ya kweli, hivyo kusababisha hatari ya madhara kwa mzungumzaji au watu wengine
  • maudhui ya sauti au picha yaliyotengenezwa kwa njia bandia kupitia matumizi ya teknolojia yanayodaiwa kuwa ya kweli, kama vile maudhui ya video au sauti ya ngono yaliyotengenezwa kidijitali au maudhui yanayodai kwa uongo kuwa mtu fulani amefanya uhalifu

Maudhui yanayojaribu kudanganya au kuingilia michakato ya uchaguzi ni pamoja na, ila si tu:

  • upotoshaji wa taratibu katika mchakato wa kiraia unaoweza kukatisha tamaa au kuzuia ushiriki
  • maudhui yanayopotosha yanayotangazwa ili kuwatisha au kuwakandamiza wapigakura ili wasishiriki katika uchaguzi

Maudhui yanayojaribu kuhadaa jumuiya ya Spotify ni pamoja na, ila si tu:

  • kuchapisha, kushiriki au kutoa maelekezo kuhusu kutekeleza programu hasidi au mbinu hasidi husika zinazolenga kudhuru au kufikia bila idhini kompyuta, mitandao, mifumo na teknolojia zingine
  • kuhadaa au majaribio yanayohusiana ya kukusanya au kuomba kwa njia ya udanganyifu maudhui nyeti
  • kuhimiza ulaghai wa uwekezaji na fedha kama vile kupata utajiri wa haraka na miradi ya piramidi, au kuwahimiza wengine kutoa pesa kwa visingizio vya uongo

Maudhui Nyeti

Tuna maudhui mengi mazuri kwenye Spotify, lakini kuna vitu fulani tusivyoruhusu kwenye mfumo wetu. Usichapishe maudhui ya vurugu au ya kutisha kupita kiasi na usichapishe maudhui ya ngono dhahiri. Mambo ya kuepuka:

Maudhui yanayotangazaa maonyesho ya kutisha au yasiyofaa ya vurugu, kutapakaa damu au picha nyingine zinazotisha ni pamoja na, ila si tu:

  • miili iliyoharibika sana au iliyokatwa vipande vipande
  • kuhimiza ukatili au mateso kwa wanyama

Maudhui yenye nyenzo dhahiri za ngono ni pamoja na, ila si tu:

  • ponografia au maonyesho ya picha za sehemu za siri au uchi zinazowasilishwa kwa madhumuni ya kuridhisha kingono
  • kutetea au kusifu mada za ngono zinazohusiana na ubakaji, kujamiiana na jamaa au uhayawani

Maudhui Haramu

Sheria ni sheria. Bila kujali wewe ni nani, ni wajibu wako kutii sheria na kanuni zinazotumika. Mambo ya kuepuka:

Maudhui yanayokiuka sheria na kanuni zinazotumika ni pamoja na, ila si tu:

  • maudhui ambayo hayatii kanuni za usafirishaji nje na vikwazo vilivyopo
  • maudhui yanayolenga kuhimiza au kufanya kitendo haramu cha aina yoyote

Maudhui yanayokiuka haki za uvumbuzi za wengine ni pamoja na, ila si tu:

  • maudhui yanayotolewa kwa Spotify bila kupata ruhusa zinazohitajika
  • maudhui yanayokiuka hakimiliki au chapa za biashara za wengine

Je, Spotify inatekelezaje sheria hizi?

Spotify inajitolea kutekeleza sheria hizi bila kubagua na kwa ukubwa ulimwenguni kote kwa kutumia mchanganyiko wa teknolojia na ukaguzi wa binadamu. Pamoja na ripoti za watumiaji, tunatumia zana za kiotomatiki zinazotegemea mchanganyiko wa ishara ili kugundua maudhui ambayo yanaweza kukiuka Kanuni zetu za Mfumo.

Tuna timu za kimataifa za wataalamu wanaotunga, kudumisha na kutekeleza Kanuni za Mfumo. Maudhui yanayoweza kukiuka sera yanaporipotiwa au kugunduliwa, timu zetu zitafanya kazi ili kuchukua hatua inayofaa ya utekelezaji.

Je, nini hutokea sheria zinapovunjwa?

Huwa tunachukulia maamuzi haya kwa uzito na tunazingatia muktadha tunapotathmini ukiukaji unaojitokeza wa Kanuni za Mfumo. Kuvunja kanuni kunaweza kusababisha maudhui yaliyokiuka kanuni yaondolewe kwenye Spotify. Ukiukaji wa mara kwa mara au uliokithiri unaweza kusababisha akaunti zisimamishwe na/au zifungwe kabisa. Pata maelezo zaidi kuhusu vitendo vingine tunavyoweza kuchukua kwenye maudhui au akaunti hapa.

Ni nini kingine ninachohitaji kujua?

Kanuni hizi za Mfumo zitasaidia kuhakikisha Spotify inasalia kuwa mfumo wazi na salama kwa wote. Tutaendelea kutathmini na kusasisha maelezo haya inapohitajika, kwa hivyo tafadhali angalia tena mara kwa mara. Kulingana na bidhaa au vipengele vya Spotify unavyotumia, unaweza kuhitajika kuzingatia masharti ya ziada.

Ninawezaje kuripoti tatizo?

Je, umepata tatizo katika sehemu ya maudhui kwenye Spotify? Ikiwa ndivyo, tafadhali tujulishe kwa kuliripoti hapa.