Sheria ya Huduma za Dijitali ya Umoja wa Ulaya (DSA) ni kanuni inayolenga kupambana na maudhui haramu mtandaoni.
Ripoti ya Uwazi ya Sheria ya Huduma za Dijitali ya Spotify inajumuisha muhtasari wa mbinu zetu, ikiwa ni pamoja na sera, desturi na hatua zinazohusiana na maudhui ya watumiaji katika huduma za kati za Spotify. Ripoti hii ni muhimu kwa ajili ya kukuza uwazi na uwajibikaji.
Kanuni za Mfumo wa Spotify zinaainisha kinachoruhusiwa na kisichoruhusiwa kwenye huduma zetu. Tunafanya kazi kwa uaminifu kushughulikia maudhui haramu na yenye madhara yanayopakiwa na watumiaji huku tukilinda haki za msingi na data za watumiaji.
Ripoti ya Uwazi ya Sheria ya Huduma za Dijitali ya Spotify ya 2024 inapatikana hapa.
Kanuni za Maudhui ya Kigaidi Mtandani (TCO) za Umoja wa Ulaya (EU) zinalenga kudumisha usalama wa raia wa Umoja wa Ulaya kwa kuhitaji huduma za dijitali ziondoe maudhui ya kigaidi kwa haraka na ufanisi huku zikiheshimu haki za msingi kama vile uhuru wa kujieleza.
Spotify hufanya kazi kupambana na maudhui hatari ya kigaidi ikiwa yanapatikana kwenye mfumo. Tunashirikiana na mamlaka na washirika wanaoaminika ili kukabiliana na tatizo hili linaloikumba sekta yote na kuboresha kila wakati michakato yetu ya ndani ili kushughulikia vitisho vinavyojitokeza.
Ili kutii TCO, Ripoti ya Uwazi ya Spotify kuhusu Maudhui ya Kigaidi Mtandaoni huainisha juhudi zetu za kuzuia na kukomesha maudhui ya kigaidi kwenye mfumo wetu. Ripoti hii hutoa muhtasari wa mbinu zetu, ikiwa ni pamoja na jinsi ya kubaini na kutekeleza sheria dhidi ya maudhui ya kigaidi na kujibu maagizo ya kuondoa kutoka kwa mamlaka za kitaifa zenye jukumu hilo katika Umoja wa Ulaya.
Ripoti ya Uwazi ya Spotify kuhusu Maudhui ya Kigaidi Mtandaoni ya 2024 inapatikana hapa.