Spotify ni huduma ya muziki dijitali, podikasti na vitabu vya kusikiliza inayokuruhusu kufikia mamilioni ya nyimbo na maudhui mengine kutoka kwa watayarishi duniani kote. Tumejitolea kutoa mazingira salama na kulinda faragha ya watumiaji wetu. Ili kuwezesha jitihada hizi, timu zetu za kimataifa zinafanya kazi usiku na mchana ili kulinda watumiaji wetu kwenye Spotify dhidi ya hatari, kuweka data yao salama na kuhakikisha hali ya matumizi inafurahisha kwa kila mtu.