Kituo cha Usalama na Faragha

Faragha

Kukusanya data yako ya binafsi

Ni muhimu sana kwetu uelewe data ya binafsi tunayokusanya kukuhusu, jinsi tunavyoikusanya na ni kwa nini tunahitaji kuikusanya.

Tunakusanya data yako ya binafsi kwa njia zifuatazo:

  1. Unapojisajili kwenye Huduma ya Spotify au unaposasisha akaunti yako - tunakusanya data fulani ya binafsi ili kufungua akaunti yako ya Spotify ili uweze kutumia Huduma ya Spotify. Hii ni pamoja na jina la wasifu na anwani yako ya barua pepe, kama ilivyofafanuliwa kwa maelezo zaidi katika sehemu ya 3 ya Sera yetu ya Faragha.
  2. Kupitia matumizi yako ya Huduma ya Spotify - unapotumia au kufikia Huduma ya Spotify, tunakusanya na kuchakata data ya binafsi kuhusu vitendo vyako. Hii ni pamoja na nyimbo ulizocheza na orodha za kucheza ulizotengeneza. Hii ni aina ya Data ya Matumizi iliyo katika sehemu ya 3 ya Sera yetu ya Faragha.
  3. Data ya binafsi unayoamua kutupa - mara kwa mara, unaweza pia kutupa data ya ziada ya binafsi au kutupa ruhusa ya kukusanya data ya binafsi k.m. ili kukupa utendaji au vipengele zaidi. Hii inaweza kujumuisha aina za Data ya Sauti, Data ya Ununuzi na Malipo na Data ya Utafiti na Tafiti zilizo katika sehemu ya 3 ya Sera yetu ya Faragha.
  4. Data binafsi tunayopokea kutoka kwa vyanzo vya wahusika wengine - ukijisajili kwenye Spotify kwa kutumia huduma nyingine au uunganishe akaunti yako ya Spotify kwenye programu, huduma au kifaa cha wengine, tutapokea data yako kutoka kwa washirika hao wengine. Huenda tukapokea pia data yako kutoka kwa watoa huduma za kiufundi, washirika wa malipo na utangazaji na washirika wa utangazaji. Angalia sehemu ya 3 ya Sera ya Faragha kwa maelezo zaidi.