Kituo cha Usalama na Faragha

Vitendo vya Maudhui

Je, ni hatua gani zinaweza kuchukuliwa kuhusu maudhui?

Kuna hatua mbalimbali ambazo Spotify huchukua kuhusiana na maudhui yanayokiuka Kanuni za Mfumo, sheria husika au ambayo huenda yana mada nyeti. Hatua hizi ni pamoja na kuondoa maudhui, kudhibiti upatikanaji wa maudhui, kudhibiti uwezo wa maudhui kuchuma mapato na/au kuwekea maudhui angalizo la ushauri.

Tunazingatia vigezo mbalimbali tunapobaini hatua za kuchukua, kama vile muktadha wa mada mahususi au tukio la sasa na ukubwa na/au mara ambazo ukiukaji umejitokeza hujumuishwa kama sehemu ya mchakato wetu wa ukaguzi. Tunatumia mbinu mbalimbali za utambuzi wa binadamu na algoriti ili kusaidia kutambua maudhui ambayo yanahitaji kuchukuliwa hatua, ikiwa ni pamoja na ripoti za watumiaji. Matumizi yoyote mabaya ya michakato yetu, ikiwa ni pamoja na kuripoti kunakolenga maudhui au mtumiaji mmoja, kunaweza kuzuia uwezo wako wa kuwasilisha maombi katika siku zijazo.

Kuondoa maudhui

Ikiwa maudhui yanakiuka Kanuni zetu za Mfumo, huenda yakaondolewa kwenye Spotify.

Kuondoa akaunti

Ukiukaji wa mara kwa mara au uliokithiri wa Kanuni za Mfumo unaweza kusababisha akaunti isimamishwe au ifungwe kabisa. Kumbuka kuwa hatua hii inaweza pia kujumuisha akaunti zote zinazohusiana na Spotify zinazomilikiwa na mtayarishi.

Kudhibiti upatikanaji wa maudhui

Katika hali ambazo maudhui yanakaribia kukiuka lakini hayatimizi vigezo vya kuondolewa kwa mujibu wa Kanuni zetu za Mfumo, tunaweza kuchukua hatua za kuzuia na kudhibiti usaambaji wake. Ingawa maudhui yataendelea kupatikana kwenye Spotify, yanaweza:

  • kutostahiki kutangazwa kwenye mfumo;
  • kupunguzwa katika mapendekezo;
  • kupangwa nafasi ya chini katika matokeo ya utafutaji; na/au
  • kutojumuishwa kwenye baadhi ya vipengele vya bidhaa za Spotify.

Katika nyakati za hatari zaidi mara nyingi kuna tishio kubwa la maudhui hatari mtandaoni, kwa mfano, wakati wa uchaguzi, migogoro ya vurugu au matukio ya vifo vingi. Kwa kutambua hili, Spotify inaweza kuchukua hatua za ziada wakati wa matukio kama hayo, kama vile kuzuia ufikiaji wa aina fulani za maudhui na/au kuangazia nyenzo kwa wakati na nyenzo zinazoaminika.

Kudhibiti uchumaji wa mapato unaotekelezwa na Spotify

Si maudhui yote yanastahiki kuchuma mapato kwenye Spotify. Pamoja na Kanuni za Mfumo, maudhui ambayo ungependa kuchumia mapato yatakaguliwa kulingana na Sera zetu za Uchumaji Mapato.

Kujumuisha ushauri kuhusu maudhui

Katika hali ambazo muktadha zaidi huenda ukahitajika kuhusu mada husika, angalizo la ushauri kuhusu maudhui huenda likawekwa ili kuongeza maelezo yanayofaa na/au kuelekeza watumiaji kwenye nyenzo zinazoaminika na kwa wakati unaofaa.

Kuzuia maudhui katika nchi au eneo mahususi

Spotify ni jumuiya ya kimataifa na inaheshimu sheria za nchi tunakoendesha biashara yetu. Ni sharti watumiaji watii sheria na kanuni zinazotumika. Maudhui ambayo hayakiuki Kanuni zetu za Mfumo yanaweza bado yakawekewa vizuizi katika nchi au eneo mahususi ambako maudhui yamekiuka sheria zake.

Rufaa

Tutaendelea kupanua chaguo na uwezo wetu wa kushughulikia rufaa, unaotofautiana kulingana na eneo.

Ikiwa unaishi katika Jumuiya ya Umoja wa Ulaya na unaamini kitendo kisicho sahihi kimetekelezwa kwenye maudhui yako au kutokana na ripoti yako, tafadhali angalia arifa uliyotumiwa na Spotify kwa hatua zinazofuata.