Kituo cha Usalama na Faragha

Mwongozo wa Wazazi au Walezi

Mifumo kama vile Spotify hutoa fursa ya kipekee kwa wazazi na watoto kugundua kwa pamoja, kupata maudhui ya elimu na kusikiliza muziki. Huenda wengine wenu mlifurahia orodha za kucheza za muziki wa kubembeleza watoto ili kuwalaza watoto wenu, na wengine wengi wamefurahia kuwachezea wimbo waliokuwa wanaupenda walipokuwa watoto. Katika miaka ya hivi majuzi, kumekuwa na ongezeko kubwa mtandaoni la maeneo ambayo watoto wanaweza kutumia, na inaweza kutatiza kufahamu jinsi ya kulinda usalama wao wakati wanacheza.

sc_section_10_alex_holmes_img_alt

Mimi ni Alex Holmes, na ninahudumu katika bodi za ushauri wa usalama duniani za kampuni kadhaa kubwa za mitandao ya kijamii, nikiwashauri kuhusu mbinu zao za usalama na madhara mtandaoni, ikiwa ni pamoja na Spotify. Mimi pia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa shirika lisilo la faida la The Diana Award, urithi wa imani ya Princess Diana kwamba vijana wana uwezo wa kubadilisha ulimwengu. Nilianzisha mpango wa kusaidiana na rika wa Mabalozi wa Kupambana na Unyanyasaji nilipokuwa na miaka 16 baada ya kunyanyaswa mimi mwenyewe. Kama unavyoweza kufikiria, ninavutiwa sana na kushughulikia vizuizi vyovyote vya furaha na ustawi wa watoto.

Katika ulimwengu wa mtandaoni, huwa ninapendekeza kila wakati kuwa wazazi wanapaswa kufanya kazi pamoja na watoto wao ili kuwaweka salama. Jadili aina ya maudhui ambayo unapenda wasikilize, na wasaidie kuelewa wanachoweza kufanya iwapo maudhui haya yatawasikitisha au kuwapa wasiwasi. Kama sehemu ya dhamira yake ya kutunza usalama wa watoto, Spotify imetengeneza mwongozo unaoainisha zana na vipengele vya hivi karibuni vilivyobuniwa kwa ajili ya watoto, ikiwa ni pamoja na vidhibiti vya wazazi unavyoweza kutumia ili kuwalinda dhidi ya maudhui dhahiri na njia za kuripoti maudhui yoyote yasiyotakikana au tahadhari.

Ni vigumu kufuatilia mifumo yote tofauti ambayo mtoto wako anaweza kutumia, na ninahimiza kila mzazi au mlezi kufanya kazi na mtoto wake ili kuelewa Spotify, aina ya muziki anaosikiliza na njia anazoshirikiana na wengine. Huenda pia ikawa na manufaa kumsaidia kufikiria kuhusu vitendo vyake kwa watoto wengine na kuwa anatakiwa kuzingatia majina ya orodha za kucheza, wasifu au picha/vipakiwa vya orodha za kucheza. Mhimize kushiriki orodha zake za kucheza nawe, kwa kuwa hii inaweza kuwa fursa ya kuratibu na kuwasiliana na kuwa na mazungumzo mazuri.

Muziki na sauti ni sehemu muhimu za jinsi watoto wanavyojifunza kujieleza na kuelewa ulimwengu. Kwa usaidizi sahihi, unaweza kutumia zana kama vile Spotify kuwasaidia kuwa wabunifu zaidi, imara na wadadisi huku wakizingatia faragha yao, uhuru na mtindo wako mwenyewe wa malezi. Mwisho wa siku, kuzungumza na mtoto wako kuhusu masuala haya ndiyo njia bora zaidi ya kuonyesha kuwa unamuunga mkono anapojifunza kuhusu ulimwengu wa kidijitali.

Alex Holmes

Mtaalam wa Usalama wa Watoto

www.antibullyingpro.com

Kuunda Hali Salama ya Utumiaji kwa Vijana

Spotify ni huduma ya muziki dijitali, podikasti na vitabu vya kusikiliza inayokuruhusu kufikia mamilioni ya nyimbo na maudhui mengine kutoka kwa watayarishi duniani kote. Tunaelewa kuwa kufuatilia ulimwengu wa kidijitali kunaweza kuwa changamoto kwa wazazi na kuwa maamuzi kuhusu maudhui na hali za utumiaji ambazo zinafaa familia yako mara nyingi huwa za binafsi. Ili kusaidia upate hali ya utumiaji ambayo ni salama na ya kufurahisha, tumepanga safu ya hatua muhimu. Hizi ni pamoja na:

Kadri mazingira ya usalama wa watoto yanavyobadilika, tutaendelea kuboresha sera, zana na uwezo wetu. Kwa sasa, tafadhali soma zaidi ili upate maelezo zaidi kuhusu hatua unazoweza kuchukua kama mzazi au mlezi ili kutusaidia kuunda hali salama ya utumiaji.

Hali ya Mtoto Wako kwenye Spotify

Kufungua akaunti

Ni sharti watumiaji wote watimize masharti ya umri wa chini wa nchi inayohusishwa na akaunti zao. Ikiwa mtoto wako yuko chini ya umri wa chini unaoruhusiwa kutumia Spotify au hajatimiza Masharti yetu ya Kutumia, ni lazima akaunti yake ifungwe.

Wakati wa kufungua akaunti, ni muhimu uweke umri wa mtoto wako kwa usahihi. Hili huhakikisha utii wa sheria za mahali ulipo na hutusaidia kutoa hali ya matumizi ya bidhaa inayofaa umri wake.

Vifurushi vya Premium ya Familia

Katika masoko fulani, tunatoa hali zifuatazo kwa sasa kama sehemu ya Kifurushi chetu cha Premium ya Familia:

  • Spotify ya Watoto ni programu inayojitegemea inayotoa hali inayoratibiwa ya matumizi na inajumuisha maudhui ambayo huenda yakawavutia zaidi watoto wadogo. Ili upate maelezo zaidi, bofya hapa.

Iwe unajijumuisha katika Kifurushi cha Premium ya Familia au la, Spotify hukupa zana mbalimbali za kukusaidia kuratibu hali ya matumizi inayofaa familia yako.

Kubuni Hali Salama ya Utumiaji kwa Mtoto wako

Maamuzi kuhusu aina za maudhui zinazofaa familia yako ni ya mtu binafsi. Ili kukusaidia kuwekea mapendeleo hali ya matumizi ya familia yako, tunapendekeza uruke maudhui dhahiri au kudhibiti uchezaji wa wasanii mahususi.

Kichujio cha Maudhui Dhahiri

Watayarishi na wenye hakimiliki mara nyingi huwekea lebo maudhui ambayo huenda yana lugha ya watu wazima au mada kuwa "Maudhui Dhahiri" au huongeza lebo ya "E". Ili uruke maudhui ambayo yamewekewa lebo kuwa ni dhahiri, unaweza kufuata maagizo hapa.

Kidokezo cha Mtaalamu: Iwapo unacheza muziki kwenye kifaa kinachoshirikiwa au mbele ya mtoto (kwa mfano, safari ya barabara ya familia au sherehe ya siku ya kuzaliwa), kuwasha Kichujio chako cha Maudhui Dhahiri kunaweza kukusaidia kuepuka matukio ya aibu yasiyokusudiwa.

Kidokezo cha Kitaalamu: Wakati mwingine inawezekana kupata matoleo yanayofaa ya maudhui yaliyowekewa lebo kuwa ni dhahiri kwenye Spotify.

Ili uripoti wimbo, podikasti au kitabu cha kusikiliza ambacho hakijawekewa lebo kwa usahihi, wasiliana nasi hapa.

Kudhibiti Uchezaji wa Wasanii Mahususi

Unaweza kudhibiti uchezaji wa wasanii mahususi kwenye kifaa chako cha mkononi au kifaa cha mkononi cha wanafamilia yako wengine wa kifurushi cha Familia kwa kwenda kwenye wasifu wa msanii, kubofya vitone vitatu na kuchagua 'Usicheze hii' katika kila akaunti.

Kuwekea maudhui alama kuwa "hayanivutii"

Watumiaji wa vifaa vya mkononi wanaweza pia kutumia kitufe cha "hayanivutii" ili kudhibiti hali zao za matumizi vizuri zaidi. Maudhui unayowekea alama kuwa "hayanivutii" yataondolewa papo hapo kwenye mipasho yako midogo na hayataonyeshwa tena. Nyimbo/albamu/vipindi vingine vyovyote vya msanii/onyesho la podikasti vitachujwa pia kwenye mapendekezo ya siku zijazo.

Kuripoti Maudhui Yanayokiuka Sera

Ni sharti maudhui yote kwenye Spotify yatii sheria za mahali husika na Kanuni zetu za Mfumo. Sheria hizi zilitungwa na timu yetu ya wataalamu wa sera ya usalama kwa kutumia maoni kutoka kwa wataalamu wa usalama wa kimataifa wanaoaminika, ikiwa ni pamoja na Spotify Safety Advisory Council. Tunazo pia timu za kimataifa zenye wahudumu wanaofanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha maudhui yanakaguliwa na kuchukuliwa hatua ipasavyo.

Sera zetu na mbinu yetu ya utekelezaji haijakamilika na inabadilika kulingana na mabadiliko ya mitindo ya matumizi mabaya, mazingira ya udhibiti wa kimataifa, aina mpya za maudhui na maoni kutoka kwa washirika wetu wa usalama tunaowaamini.

Ukipata maudhui ambayo unaamini yanakiuka Kanuni zetu za Mfumo, tafadhali yaripoti kupitia fomu hii. Ili upate maelezo zaidi kuhusu chaguo zaidi za kuripoti, tembelea Kituo chetu cha Usalama na Faragha.

Faragha kwenye Spotify

Tumejitolea kulinda data ya binafsi ya watumiaji wetu, ikiwa ni pamoja na ya watoto, na tumeweka utaratibu wa kuhakikisha maelezo ya watumiaji ni salama. Baadhi ya njia ambazo tunaweza kutumia data ya binafsi ni kutoa mapendekezo katika lugha yako, kupendekeza podikasti ambayo tunafikiri huenda ukafurahia, au kukusaidia kugundua msanii mpya unayempenda.

Ili upate maelezo zaidi kuhusu jinsi tunavyotumia data yako, haki zako za faragha na chaguo, na jinsi ya kurekebisha mipangilio yako, tafadhali angalia Kituo chetu cha Usalama na Faragha na usome Sera yetu ya Faragha.