Kituo cha Usalama na Faragha

Mtazamo Wetu kuhusu Maudhui Hatari au ya Udanganyifu

Timu za Spotify zinafanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha hali ya utumiaji ni salama na inafurahisha kwa watayarishi, wasikilizaji na watangazaji. Ingawa maudhui mengi kwenye mfumo wetu yanatii sera na idadi kubwa ya muda hutumika kusikiliza maudhui yenye leseni, watu waovu huenda wakaharibu hali ya utumiaji mara moja moja kwa kushiriki maudhui danganyifu au yaliyotengenezwa kwa hila. Tunapobaini maudhui yanayokiuka Sera zetu za Mfumo, tunachukua hatua inayofaa mara moja. Soma ili upate maelezo zaidi kuhusu mbinu tunazotumia kutunza usalama kwenye Spotify.

Maudhui ya udanganyifu yanaweza kuwa katika aina nyingi, kuanzia uvumi usiodhuru hadi kampeni mbaya, za kulenga zinazoundwa ili kusambaza hofu na hatari miongoni mwa jamii. Katika ulimwengu wenye mabadiliko mitindo hii hubadilika haraka na tunatumia ujuzi wa timu zetu za ndani na washirika wa nje ili kuelewa vyema aina hizi za ghiliba.

Katika hali nyingi, aina hizi za simulizi hasidi huenda zikashirikiwa na mtu ambaye inawezekana hajui kuwa ni za uongo au zinapotosha. Na ingawa baadhi ya uongo si hatari ("mbwa wangu ndiye mwenye akili zaidi ya wote duniani"), mifano mingine mibaya hakika ni hatari ("saratani ni shere"). Neno 'habari potofu' hutumika mara nyingi kuelezea aina nyingi za maelezo yaliyotengenezwa kwa hila, ikiwa ni pamoja na maelezo yasiyo sahihi, ambayo ni maudhui yanayoshirikiwa kimakusudi na watu wenye nia mbaya ili kutilia shaka maudhui halisi.

Maudhui hatari na ya udanganyifu yana utata na ni changamano na yanahitaji tathmini ya kina sana. Tunaamini kuwa kushughulikia aina hii ya ukiukaji kupitia aina nyingi za sera kutaturuhusu kuwa na ufanisi na usahihi katika maamuzi yetu.

Kwa mfano, ndani ya sera zetu za Maudhui Hatari, tunaweka wazi kuwa haturuhusu maudhui yanayotangaza maelezo ya matibabu ya uongo au danganyifu ambayo yanaweza kusababisha madhara nje ya mtandao au kutishia afya ya umma moja kwa moja. Mfano mwingine unapatikana katika sera zetu za Maudhui Danganyifu, unaoangazia hatua tunayochukulia maudhui yanayojaribu kubadilisha kwa hila au kuingilia michakato inayohusiana na uchaguzi, ikiwa ni pamoja na yanayowatisha au kuwakandamiza watumiaji wasishiriki katika uchaguzi.

Wakati wa kutathmini aina hizi za matumizi mabaya ya mtandaoni, tunazingatia vigezo vingi, ikiwa ni pamoja na:

  • kiini cha maudhui (kwa mfano, mtayarishi anajifanya kuwa mtu mwingine?)
  • muktadha (kwa mfano, ni ripoti ya habari kuhusu simulizi hatari inayosambaa, au inaidhinisha simulizi yenyewe?)
  • motisha (kwa mfano, mtayarishi anajaribu kumlaghai mtumiaji kupiga kura kupita muda uliowekwa?)
  • hatari ya madhara (kwa mfano, kuna uwezekano mkubwa kwamba kuenea kwa simulizi kunaweza kusababisha madhara ya kimwili?)

Udanganyifu hatari mara nyingi hulenga eneo mahususi mno, hulenga masoko mahususi, lugha na watu mahususi walio katika hatari. Ili kukabiliana na hili, tunatumia utaalamu wa soko la ndani ili kuhakikisha tunafuatilia kwa karibu mitindo inayoibuka inayoweza kusababisha madhara makubwa na kukuza maarifa haya ya kibinadamu kwa kutumia viainishaji vya mashine kujifunza. Mbinu hii inajulikana kama "mtu katika mchakato."

Tunatambua kuwa aina hii ya maudhui yanaweza kuenea zaidi wakati wa vipindi vya mashaka na mabadiliko, wakati maelezo ya kuaminika yanaweza kuwa machache. Kwa sababu hii, tunaweza pia kuchukua hatua kadhaa za maudhui ili kusaidia kudhibiti kuenea kwa matumizi mabaya ya maudhui wakati wa matukio nyeti kunapokuwa na hatari kubwa zaidi ya simulizi hatarishi zinazopelekea vurugu katika hali halisi.

Kwa mfano, tunaweza kudhibiti kugundulikwa kwa maudhui katika mapendekezo, ikiwa ni pamoja na onyo la ushauri kuhusu maudhui, au kuchagua kuyaondoa kwenye mfumo. Tunaweza pia kuonyesha maudhui kutoka kwa mamlaka zinazoaminika ili kuhakikisha watumiaji wetu wana uwezo wa kufikia maelezo sahihi na ya kuaminika, kama vile viungo rasmi vya nyenzo zinazohusiana na uchaguzi zilizotengenezwa na kutunzwa na tume za uchaguzi.

Tunabadilisha mara kwa mara sera na mwongozo wetu wa wakaguzi kulingana na maoni kutoka kwa timu zetu za Spotify, wadau wa nje, na washirika wetu kwenye Spotify Safety Advisory Council.

Unaweza kusoma zaidi kuhusu kazi yetu ya usalama hapa na kuona mwongozo wetu kwa watayarishi wakati wa chaguzi zilizopita hapa.