Spotify inapania kuwapa wasanii fursa ya kujipatia kipato cha kujikimu kimaisha kupitia sanaa yao, na mamilioni ya mashabiki fursa ya kufurahia na kuhamasishwa nayo. Ili kuwezesha jitihada hizi, timu zetu za kimataifa zinafanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha hali ya utumiaji ni salama na inafurahisha kwa watayarishi, wasikilizaji na watangazaji.
Kwenye Spotify, idadi kubwa ya muda wa kusikiliza hutumika kwenye maudhui yenye leseni. Bila kujali ni nani aliyeunda maudhui, kipaumbele chetu kikuu ni kuruhusu jumuiya yetu kufurahia moja kwa moja muziki, podikasti na vitabu vya kusikiliza wanavyopenda. Hata hivyo, hii haimaanishi kila kitu kinaruhusiwa.
Spotify inakataza vikali maudhui yanayoendeleza ugaidi au itikadi kali na huchukulia hatua maudhui ambayo yanakiuka Kanuni zetu za Mfumo au sheria.
Linapokuja suala la itikadi kali, huwa tunakagua kwa umakini tabia za wahusika za kwenye mfumo na nje ya mtandao, ikiwa ni pamoja na (lakini siyo tu) tabia za vurugu na uchochezi wa vurugu. Tunafanya kazi kwa karibu na wahusika wengine ambao wana utaalamu kuhusu itikadi kali ili kuhakikisha tunafanya maamuzi sahihi zaidi katika michakato hii na kwa kuzingatia muktadha wa eneo, kanda na tamaduni.
Tunashughulikia maudhui ya itikadi kali kupitia sera nyingi, zinazojumuisha, lakini si tu:
Tunabaini maudhui ambayo huenda yakakiuka sera zetu ili yakaguliwe kwa kutumia mbinu za ufuatiliaji makini, tukitumia ujuzi wa kibinadamu na ripoti za watumiaji. Tunatumia pia maarifa ya wataalamu wengine duniani ili kufuatilia mitindo mipya ya matumizi mabaya na kuhakikisha tunaboresha mbinu zetu kila mara.
Linapokuja suala la utekelezaji, huenda tukachukua hatua mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuondoa maudhui au mtayarishi, kupunguza usambazaji na/au kuzuia uchumaji wa mapato. Wakati wa kubaini hatua ya kuchukua, tunazingatia madhara yanayoweza kutokea nje ya mtandao kutokana na maudhui. Vigezo vya ziada pia vinaweza kuwa ni pamoja na:
Vile vile, watumiaji wanapotafuta maudhui ya itikadi kali, wanaweza kuelekezwa kwenye vituo vya nyenzo vinavyotoa usaidizi kwa wale waliotumia maudhui yenye itikadi kali. Nyenzo hizi zilitengenezwa kwa ushirikiano na wataalamu wengine, ikiwa ni pamoja na Spotify Safety Advisory Council, na huwahimiza watumiaji kutathmini kwa kina maudhui wanayotumia.
Nafasi hii ni ngumu, changamani na inabadilika kila wakati. Tumejitolea kutumia maoni ili kufanya mabadiliko na kuboresha mbinu yetu ili kuzuia maudhui ya itikadi kali yasionekane kwenye mfumo wetu. Unaweza kusoma zaidi kuhusu kazi yetu ya usalama hapa.